Kiswahili Form One TIE Notes | Kitabu hiki ni cha kwanza katika mfululizo wa vitabu vinne vya Somo la Kiswahili kuanzia Kidato cha Kwanza hadi cha Nne, kilichoandaliwa mahususi kwako mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kitabu hiki kimeandaliwa kulingana na Muhtasari wa Somo la Kiswahili wa mwaka 2005 uliotolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Mada kuu katika kitabu hiki cha Kiswahili Form One TIE
Kitabu kimegawanywa katika sura tano:
- Lugha na mawasiliano,
- Aina za maneno,
- Fasihi kwa ujumla,
- Uandishi wa insha na barua, na
- Ufahamu.
Maudhui ya kitabu hiki yamewasilishwa kwa njia ya matini, kazi za kufanya, vielelezo, pamoja na picha ambazo zote zinachochea ujenzi wa umahiri unaokusudiwa kwa kila sura.
Vilevile, katika kila sura kuna mazoezi yenye lengo la kupima na kujenga uelewa pamoja na ujuzi katika somo hili. Hivyo basi, unapaswa kufanya mazoezi na kazi zote zilizopo kwenye kitabu hiki pamoja na kazi nyingine utakazopewa na mwalimu.